Friday, 23 March 2018

Mch Paul Kuria Kutoka Kenya Avunja Mbavu za Watu Kanisani Kwenye Marria...

LIVE: TAARIFA YA HABARI TBC 1 MACHI 23, 2018- USIKU

JIRANI YANGU NI NANI?

 Mpendwa rafik yangu,karibu sana katika blog yangu,kwa leo tutafakari  pamoja makala  haya ya jirani yangu ni nani?Kuna wakati Yesu aliulizwa "jirani yangu ni nani" Ndipo Yesu alipotoa mfano wa msamaria mwema.Kwamba kulikuwa na mtu aliyepigwa na majambazi akaachwa karibu kufa,kwa bahati alipita kuhani,alipomuona alipita kando( huyu ni kiongozi wa dini,)bila kutoa msaada wowote,baadaye alipita mlawi naye alipoona alipita kando bila kutoa msaada wowote.
Ndipo alipopita Msamaria (mgeni)akamuonea huruma akamsaidia. Baada ya mfano huo Yesu aliuliza nani katika hao watatu alikuwa jirani yake? jibu lilikuwa ni yule aliyemsaidia.
Fundisho la kwanza, jirani yako ni mtu yeyote anaeonekana mbele ya macho yako,si jirani wa kijiografia.Kama ingekuwa kijiografia, mlawi na kuhani wote walikuwa wayahudi hivyo kijiografia hawa wawili walikuwa majirani wa kabila moja, huyu msamaria alikuwa mgeni.Lakini aliacha kutazama ukabila,bali aliona binadamu mwenzake akiwa katika hatari yakufa akamsaidia.Maneno ya Bwana Yesu ya mpende jirani yako kama unavyojipenda yanazingatiwa hapa.Hivyo mimi na wewe tunapaswa kuwasisdia wale wenye shida kama vile chakula,mavazi,faraja, Kuna watu utakuta una nguo nyingi kiasi kwamba miaka miwili au zaidi inapita bila kuzivaa wakati huohuo kuna jirani hana nguo nzuri au ana nguo moja au mbili tu.Una chakula mpaka una mwaga lakini jirani yako hana chakukla.Je upendo upo wapi? Yafuatayo ni mafundisho tunayoweza kupata kwa msamaria
Fundisho la pili,Ibada bila matendo mema haina maana,naweza kuwa mtu wa ibada lakini jirani yangu ana shida kubwa ambayo iko ndani ya uwezo wangu.Kuhani na Mlawi walikuwa wanawahi ibada wakathamini ibada kuliko kumsaidia huyu aliyekuwa katika hali ya kufa.Kusali tu bila kuambatana na matendo ya huruma,haki na upendo ibaada hiyo haijakamilika.Katika hali ya kawaida matendo mema ni akiba hapahapa duniani na pia baada ya maisha haya.Hata tunapofanya mabaya tunaweka akiba lakini ni akiba mbaya.Tenda mema upande akiba,na kupata kibali mbele ya mwenyezi Mungu.Sikiliza wimbo wa Jenifa Mgendi wa Matendo mema ni akiba ambao upo humu kwenye blog hii.
Fundisho la tatu saidia bila kutegemea malipo au faida,Msamaria alijitoa kwa moyo wote, akatolea muda wake na fedha zake ili kumsaidia binadamu mwenzake.Leo inapotokea ajali watu hukimbilia si kwa lengo la kusaidia bali kwa kuiba,kupiga picha kwa ajili kutumakwenye  mitandao ya kijamii.Fikiria ungekuwa wewe umepata ajali ungejisikiaje upo katika maumivu makali halafu mtu anakuja kukuibia vitu au pesa.Leo tumo katika dunia ya kukosa huruma,matendo ya kikatili yanasikika kila siku.Kuna faida katika kusaidia wenye shida,faida ya kwanza unapomsaidia mwenye shida yule mwenye shida atafurahi,furaha ile atakuambukiza wewe, Katika maisha njia mojawapo yakuwa na furaha ni kuwasidia wengine,hiyo ni tiba kwa msongo wa mawazo. Swali la kujiuliza,ni mara ngapi nimetoa muda wangu au mali yangu kwa ajili ya mwenye shida.Watu wengine wanahitaji faraja zaid.
Fundisho la nne;Saidia bila ubaguzi wa rangi au dini, Huyu aliyepigwa na majambazi alikuwa myahudi,Msamaria hakuwa myahudi lakini alimsaidia bila kufuata ukabila au dini.Binadamu wote ni ndugu tuliyeumbwa na mwenyezi Mungu.Mwanadamu ameumbwa kwa mfano na sura ya Mungu.Hivyo kumtendea mema mwanadamu ni furaha kwa Mungu,kumtendea vibaya mwanadamu mwenzako ni dhambi,hata unapoacha kusaidia wenye shida wakati una uwezo wa kuwasaidia unao.
Fundisho la tano: Unapaswa kuwa msamaria mwema katika jamii unayoishi,tafuta hata mtu mmoja wa kumsaidia ,Uwe furaha kwa wasio na furaha,uwe upendo kwa wasio na upendo.Mungu alikuumba uwe zawadi kwa jamii yako.tumia vipaji ulivyopewa na Mungu kwa kuifaidisha jamii yako,na Mungu atakuinua sana atakubariki sana,kwa sababu Mungu alikuumba ili umtumkie na utumie vipaji alivyokupa kwa ajili yako na kwa ajili ya jirani yako.Jirani yako ni yeyote  mbele yako mwenye shida,bila kujali kama ni kabila lako au dini yako.Lakini katika jamii yako unayoishi unawafahamu wenye shida.Siku hizi kuna matapeli wanaojifanya wenye shida kumbe wanatumia mwanya huo kuiba.Lakini katika jamii unayoishi wapo watu kwa hakika wana shida anza na hao.Usisubiri mpaka uwe tajiri ndiyo utoe msaada.Kama utakuwa mkalimu katika hicho ulicho nacho, Mungu atakubariki atakizidisha hicho ulicho nacho.Anza kufanya utafiti katika jamii yako utaona kuna wahitaji wa nguo,chakula au wanaohitaji ushauri tu.Anza leo na maisha yako hayatakuwa yaleyale.
Nakutakia mafanikio.
Ndimi Michael Sinienga
Kwa mawasiliano
0769741978
Email sinienga2014@gmail.com

Bwana aliwaambia S Simya UASKOFUSHO JIMBO KATOLIKI SINGIDA KWAYA YA U...

Thursday, 22 March 2018

AIC MWANZA TOWN CHOIR - UTAVUNA -[BEST TANZANIA CHOIRS]

Jennifer Mgendi - Wema ni akiba

Jennifer Mgendi - nini(352p).mp4

Jennifer Mgendi - Nani kama Mungu (Official video)

Baba ninashukuru by Jennifer Mgendi

Tulia Moya By Jennifer Mgendi

Nalia - Mchimba Mashimo - Jennifer Mgendi

WARAKA WA AMANI (ESTER)

Rose Muhando Jipange Sawa Sawa

Rose Muhando Sitanyamaza

Rose Muhando Si Salama

Rose Muhando Ee Mungu Nitakushukuru

Tutamgusa || Rose Muhando Ft. Daudi || Official Video 2017

Rose Muhando Nibebe

Ee bwana unirehemu

Bernard Mukasa - Niseme Nini (Official Video)

Thursday, 15 March 2018

Mungu ni Upendo - Kwaya ya Mt Kizito Makuburi

Moyo Wa Maria Utuombee - Mt Sesilia Dodoma

Roho Yangu Yesu Inakutamani - Kwaya katoliki

Nimrudishie Bwana nini F A Nyundo KWAYA KATOLIKI

Inueni Vichwa vyenu F A Nyundo KWAYA KATOLIKI

Nalifurahi waliponiambia F A Nyundo KWAYA KATOLIKI

Mpigieni Mungu F A Nyundo KWAYA KATOLIKI

Mwimbieni Bwana wimbo mpya F A Nyundo KWAYA KATOLIKI

Enyi mataifa mtukuzeni Mungu F A Nyundo KWAYA KATOLIKI

MIMINA NEEMA_OFFICIAL VIDEO

Tua Mizigo - Jordan Singers

Tuesday, 13 March 2018

Kila Mtu Makongoro Choir Song.flv

A I C MAKONGORO VIJANA CHOIR MALIPO DUNIANI

AIC MAKONGORO KEKUNDU

Faustin Munishi Ulimi Official Video

Munishi Yesu Mambo Yote

Munishi Kazi Na Wanawake

Munishi Yesu Nakupenda

Munishi Ukimwi Na Maisha

Munishi Omba Utapewa

Kwaya Ya Mt Cecilia Yesu Njoo

Best Tanzanian SDA gospel songs Wasabato

Best Of Ziwani SDA Choir Mombasa Kenya

Ugandan Swahili SDA Songs, Heralds, Kampala Central, Hidden Treasure and...

Twawaombea

Mimi Nimewachagua - Fr. L. Malema

Umeniita Bwana SHIKWAKA DSM UJIO WA PAPA

Nijaposema Kwa Lugha

Upendo Hai Unafikiria nini Album

Sauti Ikatoka - Vijana Mwabibu Lutheran

Mpende Mungu Wako Album-Nkinga Christian Choir

WAKUPELEKA HUKUMUNI by P F Mwarabu